Jeshi la polisi Lindi lawaonya mafataki


JESHI la polisi mkoani humu limewaonya wanaume wenye tabia ya kuwarubuni na kuwaharibu kitabia watoto wa kike kuacha tabia hiyo.

Onyo hilo lometolewa leo na kamanda wa polisi wa mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga wakati wa  hafla ya kuwaapisha na kuwavesha beji wanachama wapya waliopata mafunzo ya awali ya ulinzi wa watoto wa kike,iliyofanyika katika uwanja wa Ilulu manispaa ya Lindi.

Kamanda Mzinga ambae alikuwa mgeni rasmi wa hafla hiyo, alisema hali inayoendelea mkoani humu kuhusu mwenendo wa baadhi ya wanaume dhidi ya watoto wakike ikifumbiwa macho itakuwa ni  vigumu kufikia lengo la serikali la kuwa na usawa kwa wanawake na wanaume katika nyanja za uongozi,utawala na utendaji(hamsini kwa hamsini).

Alisema kwa kuzingatia ukweli huo jeshi hilo litawashugulika kikamilifu wanaume wenye tabia hiyo bila simile. Katika hali inayoonesha kiongozi huyo wa jeshi la polisi mkoani humu alikuwa na uhakika wa kufanyika kwa  vitendo hivyo,alisema kukithiri kwa  utoro shuleni,mimba na ndoa za utotoni mkoani humu ni ushahidi wawazi kuhusu uwepo wa vitendo hivyo.

"Nitumie fursa hii kuwaonya wenye tabia hiyo waache,kwasababu hatuwaacha waendelee kuharibu maisha na kukatiza ndoto za watoto wetu wa kike,"alionya Mzinga.

Mbali na onyo hilo, kamanda Mzinga alitoa wito kwa jamii kuwa na moyo wa uzalendo na ulinzi kwa watoto kuanzia ngazi katika ngazi ya kaya bada la jukumu la kupambana na vitendo hivyo kuachiwa serikali na vyombo vyake vya ulinzi na usalama.Ikiwamo jeshi la polisi.

Nae katibu mkuu wa chama cha ulinzi wa watoto kike nchini (Tanzania Girl Guards Association), Grace Shaba,alitoa wito kwa wazazi na walezi nchini kuzingatia malezi mema ya Watoto wao na kuwaepusha na mambo yanayoweza kuwafanya waharibike kitabia.Ikiwamo matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii katika karne hii ya sayansi na teknolojia.

Shaba alisema lengo la chama hicho kuwa nipamoja na kuwajengea uwezo watoto wa kike ili wajiamini na kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi na maendeleo ya nchi.10:Kwaupande wake, kamishina wa chama hicho wa mkoa wa Lindi, Agnes Chipanda alitoa wito kwa wazazi na walezi kuwaruhusu watoto wao kujiunga na chama hicho.Kwasababu waliojiunga na kupata mafunzo wameonesha mabadiliko makubwa ya tabia.Hali inayosababisha kuwa mabalozi wazuri kwa wenzao ambao sio wanachama.

Katika hafla hiyo wanachama 230 waliapishwa na kuveshwa beji baada ya kuhtimu mafunzo ya awali

Post a Comment

Previous Post Next Post