Kwanini Kupiga Punyeto sio Jambo Baya....Hizi Ndizo Faida zake Muhimu Sana Kiafya

Ukweli ni kwamba, jambo la kujichua/kupiga punyeto limekuwepo kwa miaka mingi sana. Ni sawa kabisa na ni jambo la kawaida kama unaogopa kupiga punyeto, lakini ni vizuri ukajua kwamba watu wamekuwa wakifanya hicho unachokiogopa kwa karne nyingi sana zilizopita.

Hii inamaanisha kwamba kupiga punyeto ni jambo la kawaida kabisa ingawa kuna dhana potofu inayohusishwa na kitendo hiki. Jambo la kuvutia zaidi ni kwamba takwimu zinaonesha kwamba asilimia kubwa ya wanawake na wanaume wote wanaamua kufanya jambo hili wanapojisikia. Hatutakiwi kuwa wanafiki kwenye hili, ila tunachotakiwa ni kujua faida na hasara za kujiingiza kwenye kupiga punyeto.

Zifuatazo ni faida za kupiga punyeto kama yawezekana ulikuwa hujui kwamba jambo hilo lina manufaa:

Dawa tosha ya kukulaza

Kujishika sehemu zako za siri au kupiga punyeto inasaidia kupunguza shinikizo la damu na kusababisha kutengenezwa/kuachiwa kwa endorphins, aina ya kemikali inayohusika na kupunguza mfadhaiko (stress) na kuufanya mwili ulegee. Hii ndio sababu kwanini neva za fahamu zinatulia baada ya kumaliza jambo hili, bila kusahau hisia za usingizi zinazofuata baadaye.

Inasaidia kuzuia maumivu wakati wa hedhi

Kwa wanawake, kujiridhisha mwenyewe unapokuwa katika siku zako kunafanya mzunguko wa damu kwenye nyonga kuongezeka, jambo litalofanya maumivu yapungue. Hali unayoipata wakati unafika kileleni pia inaweza kusaidia na bila shaka inazidi starehe unayojipa kwa kutumia maji ya moto, wanawake wanalielewa vizuri hili.

Inakupa fursa nzuri zaidi kujistarehesha kimapenzi

Kama msemo unavyosema, mazoezi hufanya uliweze jambo kwa umaridadi wa hali ya juu. Washauri wa maswala ya ngono wanashauri kwamba, wanawake ambao hawajawahi kufikishwa kileleni kwa tendo la ndoa wanatakiwa kuanza kujipa raha hiyo yeye mwenyewe. Hii itawafanya waweze kuyajua vizuri zaidi maumbile yao na kuweza kujigusa sehemu ambazo zinawapa raha zaidi. Utaweza kujijua mwenyewe vizuri zaidi ikiwa ni pamoja na kiwango gani cha starehe kinaweza kukukidhi.

Inasaidia kuzuia saratani ya tezi dume

Hii yawezekana ikawa ni habari njema sana kwa wanaume wengi. Punyeto inasemwa kuwa inasaidia kupunguza hatari za kupata kansa ya tezi dume. Sumu huwa zinajikusanya kwenye mrija wa mkojo lakini kumwaga manii kunafanya sumu hizo zitolewe nje ya mwili jambo linalompunguzia mwanaume hatari ya kupata saratani hii 

Post a Comment

Previous Post Next Post