Mambo muhimu ya kufanya kabla hujaanza kufua nguo zilizochafuka

                                           



Umechoka na nguo zako kusinyaa, kupauka au kuchuja? Kuna suluhisho moja kuu: Acha kuziweka kwenye maji huku umefumba macho! Yafuatayo ni mambo 12 ya kufanya kusaidia nguo zako kudumu ziwe ni mpya au za zamani. Mambo haya unapaswa kuyafanya kwenye nguo unazotaka kufua kabla ya kuanza rasmi zoezi hilo, na haijalishi kama utazifua kwa mkono au kwa mashine.


· Kwanza kabisa soma maelekezo ya karatasi iliyopo kwenye nguo kuhakikisha kuwa haisemi kuwa nguo husika inatakiwa isafishwa kwa mafuta maalum tu (dry clean only). Wataalam wanasema kama nguo haijasema kuwa ni dry clean tu, basi unaweza kuifua kwa mafanikio kabisa nyumbani.


· Chambua nguo unazotakuta kufua. Maana yake ni Rangi za kuchuja nyingi zinaonekana kwa macho. Kama una wasiwasi jaribu eneo dogo la ndani kwa kulipaka maji, halafu chukua kipande cha pamba upafikiche. Kama rangi nyeupe ya pamba itabadilika hata kwa mbali sana, basi fahamu moja kwa moja kuwa nguo hiyo inachuja.

Tenga rangi zinazofanana pamoja, nguo kwa mfano jeans za bluu zina tabia ya kutoa maji yenye ubluu kwa mbali, kama utazichanganya na nguo za rangi nyingine bila shaka baada ya muda rangi halisi ya zile nyingine itapotea. Zaidi ya kutenganisha nguo za mwanga na zile za rangi za giza, unatakiwa pia kutenganisha nguo kwa kiwango cha uchafu, kwa mfano, huenda nguo zote ni nyeupe lakini moja ina udongo zaidi ya nyingine hapo itakubidi kutenganisha hizo mbili.

· Rekebisha matatuko. Ni muhimu kushona nguo pale palipotatuka kama vile mapindo ya magauni na suruali na pia kurudishia vifungo vilivyotoka kabla ya kuzifua.

· Hakikisha una sabuni sahihi. Endapo unafua na mikono kwa mfano, sabuni za unga na maji zinafaa zaidi kwa kuloweka nguo kuliko zile za mche. Vilevile sabuni zinazosema nguvu mara dufu unakuta kuwa kiasi kinachotumika ni kidogo kuliko zile zisizoandikwa hivyo. Ilihali zile zilizoandikwa kawaida zinafaa zaidi vitambaa laini na nyororo ambavyo havihitaji nguvu kubwa. Vivyohivyo kwa dawa za kugharisha na kuondoa madoa.

· Tafuta na shughulikia madoa nguo chafu ingali bado kavu, kabla hujaitumbukiza yote kwenye maji. Hii ina maana kwamba nguo ikiwa kavu ni rahisi doa kuonekana kwani kuna madoa yakishaingia kwenye maji yanapotelea sio rahisi kuyaona hadi pale nguo inapokuwa kavu tena.
 Hata hivyo ni vyema kukumbuka kuwa kanuni kuu ya madoa inasema yashughulikie punde baada ya kutokea. Endapo nguo unayotoa doa ni ya rangi tumia blichi ya kutoa madoa ya nguo za rangi na endapo ni nyeupe basi tumia blichi ya rangi nyeupe. Fuata maelekezo ya kwenye chupa.

· Angalia kama nguo ina pini zozote ama karatasi za bei toka dukani na uzitoe.
· Kagua mifukoni hakikisha hakuna chochote na kisha ifungue nje ndani na pia kama ni soksi zigeuze nje ndani.

· Ondoa mikanda na Kwa zile nguo ambazo zina kamba, legeza kamba zake ili kuwezesha kutakata kila mahali kwenye yake marinda na pia kuondoa mikunjokunjo.
· Tenga nguo dhaifu pembeni.
 Nguo hizi ni kama zile za ndani, soksi aina ya stocking na zile nguo zenye wavuwavu eneo kubwa.

· Geuza nje ndani nguo zote unazoona kitambaa chake au maandishi yanaweza kuharibiwa na mfikicho, kusababisha nyuzi kutokatoka na pia kusababisha mpauko.
· Fungua vifungo vyote na pia nyoosha kola
· Loweka zinazotakiwa kufanyiwa hivyo kwanza. Maji na sabuni yanatosha kuondoa uchafu mwingi hasa ule ambao haujakomaa. Hata madoa ambayo ni ya muda kiasi yanapungua pale nguo zinapolowekwa.

. Loweka nguo ambazo ni chafu sana kwenye ndoo kubwa, karai au sinki la kufulia kwa angalau saa nzima kabla hujaanza kuzifua.

Post a Comment

Previous Post Next Post