Vijana jijini Dar es salaam wametakiwa kuacha tabia ya kuchagua kazi ambayo mara nyingi imekuwa ikiwafanya wasuburi ajira kutoka serikalini na hivyo kukosa kipato cha kuendesha maisha yao.
Hayo yamesemwa na Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita alipokuwa akitoa hotuba kwenye mahafali ya kidato cha nne shule ya Sekondari Minazini iliyopo Kata ya Vijibweni, Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni.
Meya Mwita amesema kuwa vijana wengi wanachagua kazi kwa malengo ya kusubiri ajira kutoka serikalini jambo ambalo sio sawa bali wanapaswa kufanya shughuli yoyote ambayo itawaingizia kipato na kuweza kuendesha maisha yao.
Aidha Meya Mwita amewaasa wanafunzi hao wanaohitimu kufanya kazi na kuacha, kuchagua kazi kwani kazi ni kazi tu ilimradi inakuingizia kipato cha kuendesha maisha na iwe halali ambayo haivunji sheria za nchi
Post a Comment