Mshambuliaji wtegemeo wa Yanga, Ibrajim Ajibu.
MSHAMBULIAJI tegemeo wa Yanga, Ibrajim Ajibu amesema bado hajaonyesha kile kiwango anachokitaka huku akiwaambia wapinzani wao wa Ligi Kuu Bara kuwa, watamtambua msimu huu.
Ajibu ametoa kauli hiyo wakati Yanga ikiwa katika maandalizi ya mchezo wake wa leo Jumamosi wa ligi kuu dhidi ya Singida United kwenye Uwanja wa Namfua mkoani Singida.
Mshambuliaji huyo mwenye mabao matano katika ligi hiyo, amejiunga na Yanga msimu huu akitokea Simba baada ya kumaliza mkataba wake wa miaka mitatu.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Ajibu alisema ana vitu ambavyo anahitaji kuwafanyia mashabiki wa Yanga ambao wameonyesha upendo kwake tangu ajiunge na timu hiyo.
Ajibu alisema ana deni kubwa analodaiwa na mashabiki wa Yanga na kati ya hayo ni kuipa matokeo mazuri katika kila mechi watakayocheza ili kuhakikisha wanatwaa ubingwa kwa mara ya nne mfululizo.
Alisema anafurahia ushirikiano aliokuta Yanga kuanzia kwa mashabiki, wachezaji na viongozi ambao kila siku wanampa maneno mazuri ya matumaini na mafanikio ambayo yanampa morali ya kuipambania timu.
“Bado sijakionyesha kile kiwango ambacho mimi ninakitaka, kikubwa ninahitaji kuonyesha kiwango kitakachotupa Yanga matokeo mazuri bila ya kuangalia idadi ya mabao ambayo nimeyafunga.
“Kikubwa ninataka nifunge au nitengeneze nafasi ya bao kwa kila mechi nitakayocheza, hayo ndiyo malengo yangu katika kuipa mafanikio timu yangu ya Yanga.
“Ninajua ligi kuu ni ngumu kutokana na kila timu kujiandaa, hivyo nisingependa kuongea sana, tusubirie kwenye mechi,” alisema Ajibu.
Kati ya mabao 11 yaliyofungwa na Yanga ambayo ipo nafasi ya pili katika ligi kuu imefunga, matano yamefungwa na Ajibu huku akitengeneza mawili kwa Obrey Chirwa mwenye mabao matatu
Post a Comment