BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (Nemc), limesema ndani ya siku 14 kuanzia jana litaendesha operesheni ya kubomoa nyumba zote zilizojengwa kando ya Bonde la Mto Msimbazi jijini Dar es Salaam kinyume cha sheria.
Operesheni hiyo itawahusu pia wale wote waliojenga vibanda katika Bonde la Mkwajuni eneo la Magomeni wilayani Kinondoni jijini.
Mwanasheria Mwandamizi wa Nemc, Manchare Heche, akizungumza na Nipashe jijini jana, alisema watu wanaoishi katika maeneo hayo wanatakiwa kujiandaa kuondoka katika bonde hilo.
Hata hivyo, Heche alisema hawajui idadi kamili ya nyumba zitakazobomolewa lakini zinakadiriwa kuwa zaidi ya 10,000.
Alisema wanaoishi eneo hilo wanavunja utaratibu kwa kuwa ni sehemu hatarishi kwa maisha yao na kwamba tayari walishapigwa marufuku lakini baadhi wamerudi kinyemela.
"Mfano hawa wenye vibanda ambavyo vinachomoza kila kukicha katika Bonde la Mkwajuni, tulishawapiga marufuku na hapa palikuwa peupe lakini wamerudi. Sasa nawaambia wajiandae kuondoka hapa, operesheni hii itawahusu," alisema.
Operesheni hiyo imetangazwa kipindi ambacho serikali inaendelea kubomoa nyumba zilizojengwa kando mwa Barabara ya Morogoro, ikiwaathiri zaidi wakazi wa Kimara jijini.

إرسال تعليق