Yusuf Manji.
WAKILI wa utetezi katika kesi inayomkabili mfanyabiashara Yusuf Manji ya kutumia madawa ya kulevya, Hoodson Ntisiepo, amemuuliza mtoa ushahidi kutoka ofisi ya mkemia mkuu wa serikali iwapo mkojo alioupima ulikuwa ni Manji au wa polisi?
Hayo amehoji leo Jumatano, Agosti 23 katika Mahakama ya Kisutu, wakati wa kusikilizwa kwa ushahidi wa kesi hiyo.
Wakili huyo alihoji jambo hilo ili mashahidi waithibitishie mahakama kwani wakati Manji anakwenda msalani kutoa sampuli hiyo ya mkojo aliongozana na askari, jambo ambalo lilifanya wasikilizaji wa kesi hiyo waangue vicheko ndani ya mahakama.
Kesi hiyo ilikuwa imekuja kwa ajili ya kutolewa ushahidi na imeahirishwa hadi Agosti 25 mwaka huu ambapo Hakimu anayesikiliza kesi hiyo Cyprian Mkeha atakapotoa uamuzi kama mshitakiwa ana kesi ya kujibu ama la.
Ofisa kutoka ofisi ya mkemia wa serikali ambaye alikuwa akitoa ushahidi wake ameelezea namna alivyopima mkojo huo na kugundulika kuwa na chembechembe za madawa aina ya heroine ambapo.
Pia aliieleza mahakama kuwa majibu ya vipimo hivyo yanaweza kutokana na matumizi mbalimbali ya dawa zikiwemo dawa za binadamu za usingizi.
Post a Comment