Mtoto alilia kumkumbatia Messi, Uruguay

Mtoto mmoja wa Uruguay amepata bahati ya kuzungumza na kukumbatiwa na shujaa wake, Lionel Messi sekunde kadhaa baada mlinzi kumuondoa asimfike.

Mtoto huyo alifanya juhudi za kumfikia Messi, hatua chache kabla, mlinzi aling’amua nyendo zake na kumzuia. Hali iliyosababisha dogo aangue kilio kama ana msiba na Messi tayari aliliona tukio hilo.

Baada ya hapo, Messi alimuomba mlinzi huyo amruhusu mtoto huyo aende alipo na alifanya hivyo.

Mara moja, Messi alimpokea na kumkumbatia na mtoto huyo akaendelea kuangua kilio kwa nguvu akionyesha furaha yake.

Messi ametua na kikosi cha Argentina mini Montevideo kuwavaa wenyeji wao Uruguay katika mechi ya kuwania kucheza Kombe la Dunia.

Post a Comment

Previous Post Next Post