Maajabu ya shimo la mungu wilayani Newala

   
                                              




 Katika Wilaya ya Newala, mkoani Mtwara lipo shimo la ajabu lijulikanalo kama ;Shimo la Mungu' lililochukua robo tatu ya ukubwa wa wilaya hiyo.

Shimo hili linalotajwa kuwa moja ya vivutio mkoani Mtwara limesheheni hifadhi za misitu, mito, mabonde, mawe ambayo yanapendeza kwa macho pia kipo kisima cha maji Newala.

Jambo hili linawasumbua wale wanaojua historia yake ni taarifa za kutupwa kwa watoto, kupotea kwa watu wale wanaojaribu kuingia bila ruhusu, wabishi wasioamini tambiko na mambo mengine kadhaa ambayo hata hivyo ni vigumu kuyathibitisha.

Ni shimo la asili ambalo limekuwapo miaka mingi, na wenyeji wa Mji wa Newala wanaliita  ;Shimo la Mungu' kutokana na kile wanachoeleza kuwa ni maajabu ambayo hutokea yakianzia katika shimo hilo.

Miongoni mwa maajabu hayo ni yale ambayo hutokea nyakati za asubuhi kipindi cha masika ambapo upepo mkali sana huvuma kutoka lilipo shimo hilo.

Wanasema wakati mwingine hutokea moshi mzito ambao husambaa na kuufunika Mji wa Newala na kusababisha giza nene katika makazi ya watu kiasi cha watu kushindwa kuonana kwa kati ya dakika tatu na dakika saba.

Mkazi wa Newala, Sophia Saidi (90) anasema: "Sisi tumezaliwa tumelikuta, kutokana na shimo hilo kutotengenezwa na mtu yeyote ndio maana tukaliita  ;Shimo la Mungu".

Bibi Sophia kama anavyojulikana na wengine anasema anaongeza: "Sehemu hiyo huwa panatokea miujiza kama hiyo ambayo inaleta upepo mkali, mara giza hata sisi hatujuwi ni nani ambaye ana sababisha kuwe na giza kutoka sehemu ya shimo hilo hadi sehemu ya makazi ya watu".

Kutokana na umaarufu wake, eneo hilo limekuwa kivutio kikubwa cha watu ambao hufika kwa ajili ya kufanya matambiko ya jadi, ikiwa ni sehemu ya mila na desturi za wakazi wa Newala na wilaya nyingine jirani.

4 Comments

  1. Good news
    Thanx for information

    ReplyDelete
  2. Daaaah ni mkazi na mzaliwa wa Mtwara mjini but asili ya wazazi wangu hasa wa kiume ni katika kijiji cha Mnyeu, kata ya mtopwa wilayani NEWALA nimependa historian na miujiza ya shimo la mungu keep it up my boss lady the journalist

    ReplyDelete

Post a Comment

Previous Post Next Post