VIDEO: Rais Shein afuata nyanyo za Magufuli, Awapiga biti kali Mawaziri Wake


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein ameoneshwa kuchukizwa na kitendo cha Mawaziri wake kususia ziara yake.

Rais Shein amabye yuko kwenye ziara ya siku 3 katika mkoa wa mjini magharibi visiwani humo amejikuta akiwa na taarifa za mawaziri wawili tu walioomba udhuru wa kutohudhuria ziara yake huku wengine akiwa hana taarifa zao.

Ambapo alilazimika kusema "Baadhi ya Mawaziri wangu hawapo, nataka niwaone mawaziri wangu wote hapa, wapo wawili wameniaga wengine hawajaniaga, nilisema juzi pale tunguu narudia tena hii sio ziara ya mchezo hii ni ziara ya kazi, wanachokitafuta watakipata" Alisema Rais Shein.

Post a Comment

أحدث أقدم