kuu wa mkoa wa mjini Magharibi Mh. Ayoub Mahamoud amewahakikishia ulinzi na usalama wananchi wote siku ya sikukuu ya EID EL HAJJ huku akiwaelezea wananchi kufuta sheria katika siku hiyo.
Hata hivyo katika taarifa iliyotolewa na Ofisi ya mkoa huo imeeleza kuwa Katika kipindi chote cha sikukuu viwanja vitakavyotumika ni 29 katika maeneo tofauti tofauti na vyote vitakua na ulinzi na usalama katika mkoa wa magharibi ambapo imeelezwa vitalazimika kusitisha shughuli zao saa 4 usiku, na vingine saa 1 Jioni, ispokuwa .
Wilaya ya Mjini
Viwanja vya skukuu ambavyo vitatumika ni Mnazimmoja, Viwanja vya Demokrasia (Kibandamaiti), Kariakoo, Mnara wa kumbukumbu (mapinduzi square), Jamhuri Garden, Mnazi mmoja na Forodhani park mbapo viwanja hivi vyote vitaanza shughuli zake kuanzia saa 10:00 jioni na kufungwa saa 4:00 usiku.
Wilaya ya Magharibi “A”:
Viwanja vitakavyotumika ni kiwanja cha Dole, Kihinani Melinane, skuli ya Mbuzini, Jazira Kigorofani, Jazira, Skuli ya maandalizi ya Mfenesini na Zanzibar Park (Viwanja hivi vitaanza saa 10:00 na kumaliza saa 4:00 usiku.
Viwanja vyengine ni Skuli ya Maandalizi Mfenesini, Garagara, Kijichi kwagube, Stella Darajabovu, Kihinani Zantel, Skuli ya Regezamwendo na Mwakaje (Viwanja hivi vitaanza saa 10:00 na kumaliza saa 1:00 usiku)
Wilaya ya Magharibi “B”
Viwanja vitakavyotumika ni : Skuli ya Sekondari Biashara, Viwanja vya Magereza, Maungani, Kwa bamgeni Pangawe, Kiembesamaki kwa Abdalla Rashid, Kinuni, na Fumba (Viwanja hivi vitaanza saa 10:00 jioni na kumaliza saa 4:00 usiku)
Viwanja vyengine ni : Nyarugusu, Magirisi na Skuli ya Private Kwarara Progressive ambavyo vitaanza saa 10:00 jioni na kumaliza saa 1:00 usiku)
Viwanja ambavyo havikutajwa havitaruhusiwa kufanyika skukuu.
Aidha, Kwa upande wa Wilaya ya Magharibi “B” kutakuwa na kiwanja kipya cha sikukuu katika eneo la kupumzikia la fukwe ya bahari ya fumba eneo linalojengwa nyumba za kisasa za makaazi fumba.
Serikali ya Mkoa kwa kushirikiana na Idara ya Usafiri na leseni imeandaa usafiri maalum wa daladala kwa rout ya Fumba kwa lengo la kuwarahisishia wananchi kufika na kurudi katika kiwanja kipya cha skuu kiliopo fumba kwa urahisi.
Aliongeza kwa kusema kuwa ni marufuku katika viwanja vyote vya sikukuu kupiga muziki, wakati ambapo katika vilabu na kumbi za starehe wataendelea kufuata utaratibu wa muda uliowekwa na Serikali ambapo watatakiwa kupiga muziki kuanzia saa 2:30 usiku na kumaliza sa 6:00 usiku. isipokuwa holi la bwawani na ukumbi w ngalawa ambayo mwisho ni saa 8 usiku.
Hata hivyo uuzwaji wa vyakula katika viwanja vya skukuu wafanya biashara wote wafuate taratibu na miongozo iliyowekwa na serikali kupitia Mabaraza ya manispaa kwa kushirikiana na Wizara ya afya kwa kupata vibali vya kufanya biashara pamoja na kuimarisha usafi wakati wote ili kuepusha athari zinazoweza kutokea ikiwemo mripuko wa maradhi ya kipindupindu.
Pia Mkuu wa Mkoa huo alitoa nasaha kwa mkoa wa Kaskazini Unguja kwa kuwaomba wananchi wa Mkoa huo kuendelea kudumisha amani na utulivu katika kipindi hiki cha sikuu
إرسال تعليق