BIDHAA ZILIZOPITA MUDA WAKE WA MATUMIZI ZAKAMATWA MJINI MUSOMA


Idara ya afya katika halmashauri ya manispaa ya Musoma mkoani Mara kwa kushirikiana na mamlaka ya chakula na dawa TFDA kanda ya Ziwa imekamata shehena kubwa ya bidhaa mbalimbali vikiwemo vyakula na vinywaji vikiuzwa katika maduka makubwa ya mjini Musoma vikiwa vimeisha muda wake wa matumizi kinyume cha sheria.

Mratibu wa TFDA katika halmashauri ya manispaa ya Musoma mkoani Mara Bw. Dotto Tambuko,amesema kuwa bidhaa hizo zimekamatwa katika maduka mbalimbali zikiuzwa huku wauzaji wakiangalia faida zaidi bila kujali madhara yanayoweza kumpata mlaji.

Hata hivyo baadhi ya wamiliki ya maduka hayo makubwa,wamedai kuwa maafisa hao wa afya na TFDA wameendesha oparesheni hiyo kwa misingi ya chuki,huku wengine wakitishwa kutozwa faini kubwa endapo watashindwa kutoa rushwa.

Post a Comment

Previous Post Next Post