Bilioni 86 zatengwa kukarabati vituo vya afya 172 nchini.

Naibu waziri ofisi ya rais tamisemi mhe selemani jafo amesema serikali imetenga shilingi bilioni 86 kwa ajili ya ukarabati wa vituo vya afya 172 nchini huku maeneo ya kipaumbele yakiwa ni jengo la upasuaji wodi za kinamama na watoto maabara na nyumba za watumishi ili kuboresha utoaji huduma na kupunguza vifo vya kinamama na watoto.

Ukarabati huo utaanza mapema iwezekanavyo na hadi kufikia december 30 mwaka huu utakamilika huku wakuu wa mikoa na wilaya wakitakiwa kuhamasisha wananchi kujitolea nguvu kazi, kusimamia fedha hizo na makatibu tawala wakitakiwa kuwasilisha taarifa za kila mwezi kuhusu maendeleo ya ukarabati huo.

Fedha hizo zimetolewa na benki ya dunia kwenda wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto dola milioni  66 balozi wa canada kwenda tamisemi dola  milioni 22 na fedha za ndani zilizovuka mwaka wa fedha 2016/2017 bilioni 12.5 ambapo kila kituo kitapata shilingi milioni 500.

Kwa upande wao wakazi wa mji wa dodoma wamepongeza hatua hiyo ya serikali kwani itaboresha huduma za afya hasa maeneo ya vijijini ambayo yana uhitaji  mkubwa.

Post a Comment

Previous Post Next Post