Rais John Magufuli ameivunja Mamlaka ya Usimamizi wa Mji Mdogo wa
Kigamboni (KDA) na sasa shughuli zake zinahamishiwa katika Manispaa ya
Kigamboni.
Akizungumza leo Jumatano,Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, William Lukuvi amesema ametumwa na Rais Magufuli kutangaza
uamuzi huo.
"Kumekuwa na mgongano katika usimamizi wa ardhi kati ya KDA na
Manispaa ya Kigamboni, Rais ameliona hilo na kuamua kuivunja mamlaka
hiyo,"amesema.
Lukuvi amesema jukumu la KDA lilikuwa kusimamia upangaji wa mji wa Kigamboni wakati hilo pia ni jukumu la manispaa hiyo.
Lukuvi ametoa miezi sita kwa watendaji wa KDA kukamilisha
makabidhiano ya nyaraka na wao kuripoti kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya
Kigamboni.
Mapema Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa amesema mgongano
wa usimamizi wa ardhi Kigamboni ulisababisha migogoro mingi ya ardhi.
Amesema pia manispaa hiyo ina upungufu wa maofisa mipango miji.
Amesema manispaa ina maofisa mipango miji watatu badala ya saba wanaohitajika.
Post a Comment