Man Water Adai Seduce ni Wimbo wa Kawaida Sana..Ali Kiba Ana Mabomu Makali zaidi ya Seduce Kwangu

Msanii Alikiba ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Seduce me' amefunguka na kumtaka mtayarishaji wa muziki wake mpya Man Water asiwatishe watu kwa kusema kuwa kuna misiba mingine ipo ndani zaidi ya 'Seduce me'

Msanii Alikiba akiwa na mtayarishaji wa muziki kutoka Combination Sound Man Water wakiwa katika studio za East Africa Radio.

Alikiba alisema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio baada ya Man Water kusema huu wimbo mpya wa Alikiba ni mwepesi sana kwa nyimbo ambazo mkali huyo amefanya katika studio zake za Combination ambazo bado hazijatoka.
Msikilize hapa Alikiba na Man Water wakifunguka zaidi.


Post a Comment

Previous Post Next Post