Rais Magufuli Kuanza Ziara ya Siku Tatu Mkoani Arusha Kesho

Rais Magufuli Kuanza Ziara ya Siku Tatu Mkoani Arusha Kesho
Rais John Magufuli anatarajiwa kuwasili mkoani Arusha kesho kwa ziara ya siku tatu.

Akitoa taarifa hiyo ofisini kwake, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, amesema baada ya kuwasili, anatarajiwa kuzindua barabara ya KIA Mererani inayoanzia Uwanja wa ndege wa Kilimanjaro hadi mji wa Mererani mkoani Manyara.

Kwa mujibu wa Gambo Septemba 23, Rais Magufuli anatarajiwa kutunuku kamisheni kwa maafisa wa jeshi, tukio litakalofanyika katika uwanja wa Shekh Amry Abedi jijini Arusha.

Pia amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi siku hiyo kuhudhuria sherehe hizo.

Sherehe hizo ambazo kwa kawaida hufanyika katika chuo cha maafisa wa jeshi cha TMA, zinafanyika kwa mara ya kwanza katika uwanja huo jambo ambalo linatoa fursa kwa wananchi wa Arusha kushuhudia

Post a Comment

أحدث أقدم