Tambwe Na Chirwa Warudi Jangwani

WASHAMBULIAJI wa kutumainiwa wa Yanga, Obery Chirwa pamoja na Amissi Tambwe leo hii wataungana na kikosi hicho katika mazoezi ya kujiandaa na mechi yao ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Njombe Mji katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Washambuliaji wa Yanga  Amissi Tambwe na Obery Chirwa
Yanga na Njombe Mji zitapambana Jumamosi hii katika Uwanja wa Sabasaba mijini Njombe baada ya Shirikisho la Soka Tanzania kuifanyia mabadiliko ratiba ya ligi kuu ambapo awali ilikuwa zipambane Jumatano hii. Kitendo hicho cha nyota hao kujiunga na kikosi hicho kimepokelewa kwa mikono miwili na viongozi wa benchi la ufundi la timu hiyo baada ya kuwakosa kwa kipindi kirefu kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya goti.

Majeraha hayo yaliwafanya wawe nje ya uwanja kwa kipindi kirefu huku wakishindwa kuitumikia timu yao hiyo katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba lakini pia ule wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Lipuli FC. Mechi zote hizo Yanga haikufanya vizuri. Akizungumza na Championi Jumatatu, Daktari wa Yanga, Edward Bavu, alisema kuwa wachezaji hao kwa pamoja leo hii wataanza mazoezi baada ya kupona majeraha yao.

“Hakika tunamshukuru Mungu kwa hilo kwani wamerejea katika kipindi muafaka baada ya kupona majeraha yao ya goti. “Kwa hiyo, mpaka kufikia hapa kazi iliyobakia ni kwa makocha kuhakikisha wanawapatia mazoezi ya ufiti kabla ya kuanza kuwatumia katika mechi zijazo,” alisema Bavu na kuongeza: “Wachezaji ambao tutaendelea kuwakosa kikosini kwetu ni kipa Beno Kakolanya na Geofrey Mwashiuya ambao wote bado ni majeruhi na wanaendelea na matibabu.

Post a Comment

Previous Post Next Post