Walemavu waiomba serikali kusimamia mahitaji yao



SERIKALI imeombwa kufualitia utezalezaji wa maagizo yake kuhusu makundi yenye mahitaji maalumu ili yatekelezwe kikamilifu na halmshauri nchini.

Wito huo umetolewa leo na katibu wa Kituo cha Sanaa na Utamaduni wa Viziwi Tanzania (KISUVITA), Jaafari Muntanzary alipo zungumza na waandishi wa habari   wakati wakati anafanya usafi katika soko kuu la Lindi, ikiwa ni siku ya kwanza ya maadhimisho ya wiki ya viziwi duniani.

Muntanzary ambae aliishukuru na kuipongeza serikali kuhusu mipango, mikakati na jitihada kubwa dhidi ya makundi yenye mahitaji maalumu,alisema pamoja na nianjema iliyonayo serikali,lakini baadhi ya halmashauri kupitia idara zake maendeleo ya jamii zinakwamisha jitihada hizo.

Muntanzary ambae pia ni mwenyekiti wa KISUVITA wa mkoa wa Lindi,alisema licha ya baadhi ya wakurugenzi kupitisha na kuidhinisha maombi mbalimbali yanayoombwa na kituo hicho,lakini wakuu wa idara za maendeleo ya jamii wanakwamisha bila sababu za msingi.Huku halmashauri nyingine zikisema hazina bajeti za walemavu.Hivyo kushindwa kuchangia hata maadhimisho hayo muhimu.

Alibainisha kwamba ili serikali iweze kufikia azima yake ya kuyawezesha makundi hayo ili yaweze kushiriki kikamilifu ujenzi wa uchumi na maendeleo ya nchi,hainabudi kuzifutilia na kuzitupia macho halmashauri ili zitekeleze maagizo yake kikamilifu.

" Serikali iweke kipaumbele kwa kufutilia yanayofanyika huku chini,kwasababu hiyo sio hisani bali niwajibu wake wa msingi.Sheria namba kumi ya haki ya watu wenye ulemavu inajieleza na hata mkataba wa umoja wa mataifa umeweka na kubainisha haki hizo," alisema Muntanzari.

Mbali na hayo katibu huyo alitoa wito mwingine kwa serikali kuongeza idadi ya walimu wa lugha ya alama ili kurahisisha mawasiliano pindi walemavu wasio sikia waweze kuhudumiwa kikamilifu.Kwamadai kwamba kumekuwa na mawasiliano hafifu baina ya watoa huduma na walemavu.Hali ambayo inasababisha wakose baadhi ya haki zao za msingi.

"Kipo chuo cha Patandi,lakini walimu niwachache sana,hawatoshi.Nivema pia  taasisi za umma zipeleke watu wake wakasome ili wawe wakalimani,kwa mfano polisi na wauguzi,"aliongeza kusema.

Maelezo ya Muntazary yaliungwa mkono na ofisa wa lugha ya alama wa kituo hicho,Nassiria Nassiry kuna kila sababu ya kuwa na walimu wanaojua lugha   ya alama katika ngazi zote za elimu.Huku akitoa wito kwa jamii kushiriki kikamilifu maonesho hayo.
                       
Kwa upande wake diwani wa kata ya Ndoro,Issa Luono  ambae alikuwa bega kwa bega na walemavu hao kufanya usafi sokoni hapo,alisema lugha ya alama hajaipewa uzito na kufanywa lugha rasmi yakufundisha katika maeneo ya kutolea elimu. Hivyo kuna haja ya kuanza kufundishwa ili kurahisisha upatikamaji huduma kwa walemavu wa usikivu.

Huku pia akitoa wito kwa jamii kuwa karibu na makundi hayo yenye mahitaji maalumu ambayo yanahisi yametengwa na kujiona hayana thamani.11:Kilele cha maadhimisho hayo ambayo kwa kanda ya kusini yataishirikisha mikoa ya Lindi,Mtwara na Ruvuma kitakuwa tarehe 30 mwezi huu katika manispaa ya Lindi.

Post a Comment

أحدث أقدم