Unyonyeshaji wa maziwa ya mama ni njia mojawapo ya mafanikio makubwa kabisa ya kufanikisha na kuhakikisha afya ya mtoto anaishi vyema.
Kama kila mtoto alienyonyweshwa maziwa ya mama kwa ndani ya saa moja toka azaliwe,
upewaji pekee maziwa ya mama kwa miezi ya sita ya kwanza katika uhai wa mtoto, na kuendelea kumnyonyesha hadi umri wa miaka miwili, karibu watoto 800 000 itawasaidia kuokoa maisha yao kila mwaka. duniani, chini ya asilimia 40 ya watoto wachanga chini ya umri wa miezi sita hawapewi maziwa ya mama.
Ushauri na nasaha wa kutosha kuhusu kunyonyesha na huduma ni vitu muhimu kwa ajili ya akina mama na familia katika kuanzisha na kudumisha zoezi hili la kunyonyesha.
Shirika la afya ulimwenguni lipo kikamilifu katika kukuza hali ya unyonyeshaji kama chanzo bora cha chakula kwa ajili ya watoto wachanga na watoto wadogo.
katika makala hii nitaonyesha ukweli unaohusu faida nyingi za kufanya, na kutoa msaada sahihi jinsi akina mama wanavyoweza kuongeza kasi ya unyonyeshaji maziwa ya mama duniani kote.
Shirika la afya ulimwenguni (WHO) linapendekeza :
WHO inapendekeza kunyonyesha maziwa ya mama pekee kwa miezi sita ya kwanza katika maisha ya mtoto. Katika miezi sita, vyakula, kama vile matunda kama parachichi, ndizi na mboga, lazima aanze kuwekewa ili kumsaidia katika kipindi anachokuwa akinyonya kwa muda wa miaka miwili au zaidi.
Aidha:
- kunyonyesha unapaswa kuanza ndani ya saa moja baada ya kujifungua.
- kunyonyesha lazima kuwe"kwenye mahitaji", kama mara kwa mara kama mtoto anavyohitaji iwe mchana ama usiku; na
- unyonyeshaji wa chupa hauna budi ziepukwe.
FAIDA ZA AFYA KWA WATOTO WACHANGA
Maziwa ya mama ni chakula bora kwa watoto wachanga na watoto wakuao. pia huwapa watoto wachanga virutubisho wote wanahitaji kwa ajili ya maendeleo ya afya zao.
Maziwa haya ni salama na yana kinga ambayo husaidia kuwalinda watoto wachanga dhidi ya magonjwa ya kawaida katika utoto kama vile kuhara na pneumonia, Ambavyo ndio Sababu kuu mbili za msingi za vifo vya watoto wachanga duniani kote.
Maziwa ya mama hupatikana kwa urahisi na kwa bei nafuu (bure), ambayo husaidia kuhakikisha kwamba watoto wachanga kupata lishe ya kutosha.
FAIDA KWA AKINA MAMA
Kunyonyesha pia kuna faida kwa mama. kunyonyesha maziwa ya mama inahusishwa na njia ya asili kama njia ya uzazi wa mpango (asilimia 98 huwasaidia katika katika miezi sita ya kwanza baada ya kuzaliwa katika kuzuia mimba).
Pia inapunguza hatari ya kupata saratani ya matiti na ovaria baadaye katika maisha, husaidia wanawake kurudi katika maumbile yao kama kabla ya ujauzito, na husaidia kupunguza viwango vya unene uliopitiliza.
Faida za muda mrefu kwa ajili ya watoto
Kwa zaidi kuna manufaa ya kwa ajili ya watoto, kwa kunyonyesha maziwa ya mama inachangia kuwa na maisha yenye afya njema.
Vijana na watu wazima ambao walikuwa wananyonya maziwa ya mama walipokuwa watoto wana uwezekano mdogo sana wa kuwa na tatizo la unene na uzito uliopitiliza.
Pia huwa wako katika hali nzuri ya kutokupata uwezekano wa kuwa na aina ya 2 ya ugonjwa wa kisukari na vile vile katika kipimo cha akili huwa wako vizuri.
KWA NINI WATOTO WACHANGA WASITUMIE MAZIWA YA KOPO/FORMULA ?
Maziwa ya kopo/formula kwa watoto wachanga huwa hayana kingamwili /antibodies ambayo hupatikana katika maziwa ya mama tu. Wakati ambapo maziwa ya kopo/formula hayakutayarishwa vizuri, kuna hatari inayotokana na matumizi ya maji yasiyokuwa safi na salama na pia kutokuwa na vifaa vya kutakasia/ unsterilized au kuwepo uwezo wa bakteria katika formula ya unga hayo.
Utapiamlo inaweza kusababishwa kutokana na uchanganyaji wa maziwa ya unga na maji mengi kuliko kipimo. Kama utaweka mazingira ya kumnyonyesha maziwa ya unga kila siku mara kwa mara siku zote, na ikitukia siku hayapo maziwa hayo, na ukawa huna budi kurudi katika kumnyonyesha maziwa ya mama, basi changua hilo halitakuwa sahihi kwa sababu kutakuwa na upungufu wa uzalishaji wa maziwa katika matiti ya mama kwa siku hiyo.
VVU NA KUNYONYESHA
Mama mwenye virusi vya UKIMWI anaweza kupitisha maambukizi kwa mtoto wake wakati wa ujauzito, kujifungua na wakati wa kunyonyesha.
Dawa za Kurefusha maisha kwa wagonjwa wa UKIMWI (ARV) anayopewa mama au mtoto alie katika hatari ya kuambukizwa VVU ili hupunguza hatari ya maambukizi hayo.
Kwa pamoja, kunyonyesha na matumizi ya dawa za ARVs kuna uwezo wa kasi na mkubwa katika kuboresha nafasi ya watoto wachanga ya kuishi wakati ambapo hubaki akiwa ambaye hajaambukizwa VVU.
Shirika la Afya Ulimwenguni/WHO inapendekeza kwamba wakati mama mwenye maambukizi ya VVU kunyonyesha, anapaswa kupokea dawa za ARV na kufuata mwongozo wa shirika la afya ulimwenguni unavyosema kwa ajili ya kuwalisha watoto wachanga na sambaba na kufata ushauri wa matatibu walio karibu katika kliniki.
TARATIBU ZA KUSIMAMIA MAZIWA MBANDALA
Kanuni za kimataifa za kudhibiti masoko ya maziwa mbadala ilipitishwa mwaka 1981 ilikuwa na wito huu:
- Maandiko yote katika maziwa ya kopo/ formula na habari za kuelezea hali ya faida ya kunyonyesha maziwa ya mama na hatari ya afya ya maziwa mbadala/ yakopo au unga lazima zielezwe;
- Si ruhusa kufanya promotion ya maziwa mbadala /maziwa ya kopo ama unga;
- Si ruhusa sampuli yeyote ya maziwa mbadala kutolewa kwa wanawake wajawazito, mama au familia zao; na
- Si ruhusu kusambaza maziwa mbadala/maziwa ya kopo ama unga ya bure au ruzuku kwa wafanyakazi wa afya au na vituo vya afya.
MSAADA KWA AJILI YA AKINA MAMA NI MUHIMU
Unyonyeshaji una hitaji kujifunza na wanawake wengi wanapambana na magumu mengi sana mwanzoni wanapoanza hatua hii. Maumivu ya chuchu, na hofu kwamba hakuna maziwa ya kumtosheleza mtoto ni ya kawaida.
Vituo vya afya ambayo vinaunga mkono kunyonyesha hufanya mafunzo juu ya kunyonyesha sambamba na upatikana wa ushauri kwa mama wapya katika kunyonyesha hii huhamasisha viwango vya juu katika uzoefu katika kunyonyesha.
Kutoa msaada huu na kuboresha huduma kwa akina mama na watoto wachanga, kuna hatua kadhaa zimetolewa kama"mama na mtoto" katika kliniki Nchini kwetu katika mpango huo ushauri na taratibu za unyonyeshaji hutolewa pale.
KAZI NA KUNYONYESHA
Akina mama wengi ambao kurudi kufanya kazi makazini kwao wengi wao huachana au kunyonyesha kwa muda watoto wao au kabisa wengine kuacha kuwanyonyesha. sababu kuu ikiwa ni hawana muda wa kutosha, au mahali pa kukaa na kunyonyesha, hujieleza kwa kukosa kuhifadhi ya kusitiri maziwa yao.
Akina mama wanahitaji usalama, hali ya usafi na sehemu ya kujisitiri au sehemu ya karibu na mahali pa kazi yao kwa kuendelea kunyonyesha. na pia ili Kumwezesha kuendelea na kazi zake, wengi wao hulazimika kuomba likizo ya kulipwa ya uzazi, vifaa vya kwa ajili ya kutoa na kuhifadhi maziwa kwenye matiti, wengi wao hii huwasaidia.
HATUA YA PILI: KUMUANZISHIA CHAKULA KIGUMU MTOTO
Ili kukidhi mahitaji ya kuongezeka kwa watoto katika umri wa miezi sita, chakula kigumu lazima kiazishwe ili kusaidia wakati akiendelea kunyonya kwa muda huo.
Cha Vyakula cha mtoto kinaweza kuwa ama kuchukuliwa hasa kutoka milo familia kwa watu wakubwa kadiri inavyowezekana.
Wataalamu wa afya na vyakula wanasema ya kwamba,
- Kunyonyesha hakupaswi kupungua wakati unaanza kumpatia chakula kingine kigumu;
- Chakula apatiwe mtoto ama itolewe na kijiko au kikombe/sahani na si katika chupa;
- Chakula lazima kiwe safi, salama na kipatikane katika mazingira zilizopo; na
- Na muda wa zaidi na wakutosha unahitajika kwa ajili ya watoto wadogo kujifunza kula vyakula vingine vigumu.
إرسال تعليق