Kamati ya Zabuni ya Simba Kumtangaza Mwekezaji Mpya Leo?

Kamati ya Zabuni ya Simba Kumtangaza Mwekezaji Mpya Leo?


 

Klabu ya Simba huenda leo ikaingia kwenye ukurasa mpya wa uendeshaji wa timu ambapo kamati maalum ya kusimamia mchakato wa zabuni ya kumpata mwekezaji kwenye muundo mpya wa klabu ya hiyo leo Saa 5:00 asubuhi inatarajiwa kukutana na Waandishi.

Taarifa ya Simba SC kwa vyombo vya Habari iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu, Hajji Sunday Manara imesema kwamba mkutano huo utafanyika kwenye ukumbi wa Kivukoni 3 uliopo ndani ya hoteli ya Serena mjini Dar es Salaam.
Kamati hiyo iliyoundwa mapema mwezi uliopita, ipo chini ya Mwenyekitil, Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu Thomas Mihayo na Wajumbe wengine wanne, ambao ni Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan ‘Zungu’, Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, Abdul-Razaq Badru, Wakili Dk. Damas Ndumbaro na Yusuph Maggid Nassor.
Agosti 20, mwaka huu wanachama 1,216 wa klabu ya Simba waliridhia mfumo wa klabu yao kuuza Hisa baada ya Mkutano uliofanyika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Nyerere (MNICC), Dar es Salaam.

Katika mkutano huo uliohudhuriwa na Waziri wa Afya Jinsia na Watoto, Dk Hamisi Kigwangala, Kaimu Mwenyekiti wa klabu, Salim Abdallah 'Try Again' alisema kwamba asilimia 50 ya hisa zitauzwa kwa mwekezaji au wawekezaji watakaoungana wasiozidi watatu, kwa sharti moja tu la kuwa wanachama wa klabu hiyo.  Mwekezaji anatakiwa kuweka dau lisilopungua Sh. Bilioni 20 ili kupatiwa asilimia 50 ya hisa za klabu, wakati kwa kuanzia wanachama wote wa Simba wamepewa asilimia 10 ya hisa. 

Post a Comment

Previous Post Next Post