Korea Kaskazini: Kim Jong-un ampandisha cheo dada yake mdogo


Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un, amempandisha cheo dada yake mdogo, na kumpa madaraka zaidi katika chama tawala cha wafanyakazi.

Kim Yo-jong, anayeaminika kuwa na umri wa zaidi ya miaka 26 amekuwa mjumbe katika kamati kuu ya chama, ambalo ni baraza kuu la uamuzi linalojulikana kama politburo.

Bi Kim Yo-jong alipewa kwanza wadhifa wa kuwa afisa wa wa cheo cha juu wa chama, miaka mitatu iliyopita.

Familia ya Kim, imeongoza Korea Kaskazini, tangu nchi hiyo ilipoundwa, mwaka wa 1948

Post a Comment

Previous Post Next Post