WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO, DK. HARRISON MWAKYEMBE.
Kauli hiyo ilitolewa juzi na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, baada ya timu ya soka ya vijana ya Wasichana ya Taifa (Tanzanite) kupokea kichapo cha mabao 6-0 kutoka kwa wenzao wa Nigeria.
Kwa matokeo hayo, Tanzanite imeiaga michuano hiyo ya kusaka tiketi ya kucheza fainali za dunia, kwa jumla ya mabao 9-0 kutokana na awali ugenini kufungwa 3-0 katika mechi ya kwanza iliyofanyika Nigeria wiki mbili zilizopita.
Waziri Mwakyembe alisema kwa kuanzisha mashindano ya Kombe la Taifa kwa wasichana/wanawake kutasaidia kuibua na kuimarisha vipaji vya nyota hao wa hapa nchini.
Waziri huyo alisema kuwa bila kuwekeza katika mashindano ya vijana, kupata matokeo mazuri itakuwa ni historia, hivyo anawaomba wadau kushirikiana na serikali kuwekeza kwenye mashindano ya vijana.
"Kwa upande wa wanaume kwa sasa nimeanza kuridhishwa na maendeleo yake, vijana wametafutwa kutoka sehemu mbalimbali za nchi na wanafanya mazoezi mara kwa mara, lakini huku kwa wasichana bado, naomba tushirikiane kuinua soka la wanawake," alisema Waziri Mwakyembe.
Aliwataka pia wazazi na jamii kuwapa ushirikiano watoto wa kike ambao wanacheza soka na kutowachukulia kuwa ni vijana waliopotea katika maisha.
Naye Kocha Msaidizi wa Tanzanite na Twiga Stars, Edna Lema, alisema kukosekana kwa mechi za kirafiki za kimataifa kumesababisha timu hiyo kufanya vibaya na kulitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutochoka kuwatafutia michezo ya kujipima nguvu
إرسال تعليق