Tarehe 15 Oktoba 1987, Thomas Sankara, rais wa Burkina Faso, aliuawa kwa kupigwa risasi na kundi la askari walioasi. Miaka thelathini baadaye, wakazi wa mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou, bado wana kumbukumbu ya mauaji hayo. Watu wengi wamekua wakijiuliza maswali bila majibu.
Wakizungumza na RFI wale walioshuhudia tukio hilo, wakati wa mauaji na kisha mazishi ya mwasisi wa mapinduzi. RFI imejaribu kukutana na wale ambao pia waliona mvutano kati ya marafiki wawili wa karibu, Thomas Sankara na Blaise Compaoré. Wametoa ushuhuda wao kwa kile kilichotokea, mjini Ouaga, mwaka huo wa Mapinduzi.
Siku ambayo Sankara aliuawa
Alhamisi, tarehe 15 Oktoba 1987, saa 10 jioni. Mkutano wa baraza la maridhiano ulianza mjini Ouagadougou, katika moja ya sehemu za jengo la "Burkina". Thomas Sankara litenga jengo hilo kama makao makuu ya Baraza la Taifa la Mapinduzi (CNR). Mkutano ulilenga kuundwa kwa chama kimoja cha siasa, chama kimoja pekee ambapo lengo ilikua kukusanya vyama vyote vya mrengo wa kushoto ili kuokoa zoezi la mapinduzi na kukabiliana na ongezeko la maandamano. Wajumbe sita wa baraza lake la mawaziri walikuepo.
Paulin Babou Bamouni, mwandishi wa habari, mkurugenzi wa vyombo vya habari vya rais ,Bonaventure Compaoré, mfanyakazi katika ikulu ya rais, Frédéric Kiemdé, Mshauri wa masuala ya sheria katika ikulu ya rais, Christophe Saba, katibu wa kudumu wa CNR, mshirika wa karibu na msiri wa Rais, Patrice Zagré, Muhadhiri wa Falsafa na Alouna Traoréambaye alikua akifanya kazi kama mshauri anayehusika na masuala ya mikusanyiko ya wengi katika ikulu ya rais, na ndiye pekee aliyeonusurika katika mkutano huo.
Thomas Sankara alifika katika jengo la "Burkina" baada ya kuchelewa kidogo. Alouna Traoré, ambaye alikua akirudi kutoka katika ziara ya kikazi nchiniBenin, alianza kuzungumza wa kwanza. Muda mchache milio ya risasi ilisikika pembezoni ya jengo la "Burkina".
Alouna Traore alikua hana taarifa yoyote, lakini risasi hizo zilikua zikifyatuliwa na kundi la askari waliokua walipiga kambi pembezoni mwa jengo ambapo mkutano kulikua kukifanyika mkutano. Kundi hili la askari waliwaua kwa risasi walinzi wa Thomas Sankara, kikosi chake cha karibu cha walinzi.
"Ondoka! Ondoka! Ondoka! ", waliwasihi washambuliaji kwa wale waliokua katika jengo hilo:
"Msiondoke, wanatafuta mimi", alisema Thomas Sankara, akiinuka, kwa mujibu wa Alouna Traoré.
Sankara alitoka wa kwanza nje huku akiweka mikono kichwani kama ishara ya kujisalimisha, kwa ujibu wa Alouna Traore. Mara tu alipigwa risasi. Kisha wengie walitoka nje mmoja baada ya mwengine kupitia mlango mmoja kwa amri ya wauaji. Katika ushahidi wake, Alouna Traore anasema: "Wale wote ambao walitoka njewaliuawa kwa risasi na kundi hilo la askari.
Alouna Traoré alitoka wa mwisho katika jengo hilo. "Nilikwenda kulala kati ya wale waliokuwa wameuawa," alisema. Kisha akasikia mmoja wa wauaji: "Kuna mtu ambaye hajafa, lazima apelekwe kwenye sehemu waliokua wakifanyia mkutano - [ambapo wengine wa CNR wamepelekwa]." Alimfuata, akifikiri kwamba saa yake ya mwisho imefika. "Nilimuomba mtu huyo ambaye alikuwa akinipeleka ruhusa ya kwenda haja, baada ya hapo nilijiambia kuwa wakati wangiu wa kufa umefika. Lakini hapana! Aliniongoza kwa upole kwenye chumba ambako nilikutana na wenzangu katika Baraza la usuluhishi. Tulikaa katika chumba usiku wote. Kesho asubuhi, kwa nia nzuri, tuliombwa kwenda nyumbani.
Miaka thelathini baadaye, Alouna Traoré bado hajui kwa nini alinusurika siku huyo.

إرسال تعليق