RAIS John Pombe Magufuli alitia mkono kwenye tamasha ya Fiesta jana usiku na kuamsha shangwe kwa mashabiki waliokuwa wamefurika katika viwanja vya Leaders Club Dar es Salaam! Unajua ilikuwaje? Siku chache zilizopita tamasha hilo lilipewa kibali cha kumalizika saa saba usiku, baadaye likapewa muda mpaka 11 lakini ghafla Magufuli akaamuru limalizike saa 12 asubuhi ya leo.
Majira ya saa 11, alfajiri, wakati msanii Chege Chigunda 'Mtoto wa mama Saidi' akiwa jukwaani akitumbuiza kwa wimbo wa 'Mwanayumba' watangazaji wa Clouds, B dozen na Adam Mchovu walimsimamisha na kuanza kuwatangazia mashabiki kuwa, wamepokea simu kutoka kwa Rais John Pombe Magufuli, kuwa anataka tamasha la Fiesta liendelee hadi saa 12.
Rais alisema kuwa alitaka wakati yeye anaenda kanisani apishane na watu barabarani wakiwa wanatoka katika tamasha hilo.
Hali hiyo ilizua shangwe kwa wapenzi wa burudani ambao walisikika wakiimba; “Magufuli, Magufuli, Magufuli.”
Ilikuwa ni kama mashindano! Wasanii waliopanda jukwaani kila mtu alitaka kumfunika mwenzake. Ubunifu ulikuwa wa hali ya juu. Baadhi ya wasanii walioonyesha ubunifu ni pamoja na Ben Pol. Msanii huyo alipanda jukwaani na muigizaji anayejulikana kwa jina la Tausi akiwa amevaa shela nyeupe na Ben Pol akiwa amevaa suti nyeupe huku wakisindikizwa na wimbo unaoitwa 'Nimekuchagua wewe' wa mwanamuziki Bob Rudala.
Huku wakiendelea wimbo huo, mara Ben Pol akabadilisha wimbo akaimba wimbo wake wa 'Sofia' lakini safari hii akabadilisha jina na kusema ‘Tausi’, mara akabadili wimbo na kuimba 'Moyo Mashine' na ghafla muigizaji wa kike wa vichekesho Ebitoke akatua jukwaani na kuanza kurushiana maneno na Tausi akidai kuwa Ben Pol ni mpenzi wake. Tukio hilo lilikuwa zuri na liliwafurahisha mashabiki.
Msanii mwingine Jux, yeye aliingia jukwaani na Vanessa Mdee na kuimba wimbo wa mwanamuziki Bushoke aliomshirikisha K-lynn 'Nalia kwa furaha' ambapo walikuwa wanapokezana maneno, lakini Vanessa alikuwa anaigiza kama vile hamtaki Jux.
Jux aliendelea kutoa ubunifu pale alipompandisha mwanamuziki Kassim Mganga ili amsaidie kumbembeleza Vanessa aweze kumsamehe ndipo alipoimba wimbo wake wa 'Haiwezekani' akimaanisha haiwezekani Vanessa amuache Jux.
Kama haitoshi Jux akampandisha Q Chillah na kuanza kumuimbia Vanessa wimbo wa 'Nikilala Naota' hapo ndipo Vanessa akatamka kuwa kamsamehe Jux na warudiane rasmi ila asirudie tena.
Pia mwanamuziki Barnaba hakuwa nyuma katika ubunifu, yeye alipanda jukwaani akiimba wimbo wa Fally Ipupa ‘Eloko Oyo’ na baadae akampandisha Isha Mashauzi na wimbo wake 'Nimpe Nani', wakaanza kuimba pamoja. Kitu hicho kiliwafurahisha mashabiki ambao walilipuka kwa furaha.
Mbali na hao, wanamuziki wengine, Roma na Stamina wao waliingia wakiwa wamevaa jezi kadhaa na kuanza kuvua moja moja huku wakibishana..
إرسال تعليق