Mawaziri wawekwa kizuizini Catalonia


Raia wa jimbo la Catalonia wanaotaka kujitenga wameandamana nje jengo la bunge la jimbo hilo mjini Barcelona baada ya jaji mjini Madrid kuwaweka kizuizini mawaziri nane wa serikali ya jimbo la Catalonia.

Taarifa zinasema kuwa hadi sasa kuna jumla ya wanasiasa kumi wa Catalonia waliowekwa kizuizini nchini Hispania wakiwemo pia viongozi wa kitamaduni wawili ambao nao wanashikiliwa.

Jaji Carmen Lamela amesema kuwa aliamua kuwaweka kizuizini viongozi hao nane kwa kuhofia kwamba wanaweza kutorokea nje ya nchini ama kuharibu ushahidi.

Waendesha mashitaka wanawatuhumu wanasiasa hao kwa makosa mawili ambayo ni mapinduzi na uchochezi katika jaribio la kutaka kujitenga na Hispania.

Hata hivyo jaji bado hajatoa kibali cha kukamatwa nje y nchi kwa kiongozi wa watu wa jimbo la Catalonia Carles Puigdemont na wenzake wane ambao wote wapo nchini Ubelgiji

Post a Comment

أحدث أقدم