Mbaroni kwa kwenda kinyume na Rais Magufuli

Walimu wakuu wa shule 3 za wilayani Muheza mkoani Tanga wamekamatwa na jeshi la polisi kwa kuchukua fedha, kwa ajili ya kuwaandikisha wanafunzi wa darasa la awali na la kwanza katika shule hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Wilaya ya Muheza Bi. Mwanasha Tumbo, amesema alibaini kuwa walimu hao wanachukua fedha kinyume na agizo la Rais la kutoa elimu bure kuanzia elimu ya msingi hadi sekondari, na kuagiza kuchukuliwa hatua ikiwemo kuvuliwa madaraka na kufikishwa polisi.

Walimu hao ambao ni wa shule ya msingi Mwambao, Bi. Jackline Mjenga, Shule ya Msingi Majengo Fatuma Asaraji na wa shule ya msingi Jamhuri, Bi. Jane Mhina, walikuwa wakichukua elfu 18 kwa kila mzazi aliyekwenda kuandikisha mtoto wake shuleni hapo,.

Kabla ya hapo Mkuu wa Wilaya hiyo alishatoa agizo la katazo la kuwachangisha wazazi michango mbali mbali, wakati serikali ilishapiga marufuku kulipa fedha yoyote kuchagia elimu kuanzia shule ya msingi hadi sekondari

1 Comments

Post a Comment

Previous Post Next Post