Wananchi wa vijiji vinne vya kata ya Barayi wilayani Karatu mkoani Arusha wakiwemo wajawazito wanalazimika kutembea umbali wa zaidi ya kilometa 100, kufuata huduma muhimu za Afya ikiwemo ya upasuaji na wameiomba serikali kuwatatulia tatizo hilo wanalodai kuwa linahatarisha maisha yao
Wakizungumza na ITV iliyotembelea kata hiyo wananchi hao wamesema licha ya kuwa na zahanati inayotegemewa na watu zaidi ya Elfu ishirini (20'000) uwezo wake wa kutoa huduma ni mdogo na wamekuwa wakipewa ahadi ya kujengewa Kituo cha Afya ambayo bado haijatekelezwa.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Karatu, Waziri Morisi, amesema katika bajeti yao ya 2018/19 wameshatenga fedha zaidi ya Milioni mia moja kwa ajili ya kujenga kituo cha Afya na ujenzi unatarajiwa kuanza wakati wowote kuanzia sasa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Karatu Bw. Jubilet Mnyenye amesema pamoja na mradi huo wa Afya pia wamepitisha bajeti bilion 39.7 kwa ajili ya miradi ya maji, Elimu ,na miundombinu ambayo ikikamilika itapunguza kero nyingi za wananchi hasa vijijini.
إرسال تعليق