Muda ulokuwa nao ndio kila kitu katika maisha yako

Moja ya kitu cha thamani sana maishani  mwetu ni muda. Hata hivyo ingawa huwezi kuona muda, huwezi kuugusa muda, lakini muda unaongoza maisha yetu na kuamua maisha yetu yaweje yaani ya mafanikio au ya kushindwa?
Muda unaweza kufanya chochote kwenye maisha yako. Kama leo hii ukitumia dakika 20 tu kufanya mazoezi baada ya miezi sita mwili wako unakuwa umebadilika. Leo pia ukiamua kujifunza vitu kwa nusu saa tu, baada ya muda unakuwa mtaalamu.
Kipi ambacho hakiwezi kuleta matokeo mbele ya muda, ikiwa muda huo utatumiwa kwa busara? Muda ndio mwisho wa kila kitu, muda unasawazisha kila kitu, ‘time is a greater equalizer’. Kama unaona maisha yako magumu, jipe muda na fanya kazi kweli, kila kitu kitabadilika.
Leo hii pengine unaitwa mtu wa kushindwa, au pengine unaitwa ni mtu usiyeweza kitu, usiumie juu ya hilo, amua sasa kutumia muda wako kwa busara kuwekeza kwa uhakika katika eneo unalotaka. Miaka mitatu au mitano mbele utakuwa mtu wa tofauti sana.

Post a Comment

أحدث أقدم