Dar es salaam ndo jiji linaloongoza umati wa watu afrika mashariki

Dar es Salaam Ndo Jiji Linaloongoza kwa Idadi ya Watu Afrika Mashariki
 Wakati mradi wa majaribio ya uzazi wa mpango ‘Tupange Pamoja’ ukizinduliwa, imeelezwa Dar es Salaam ni jiji lenye wakazi wengi zaidi ukilinganisha na mengine Afrika Mashariki.

Jiji la Dar es Salaa, limedaiwa linaongoza kwa kuwa na  idadi ya watu zaidi ya milioni sita, ukilinganisha na majiji mengine.

Hata hivyo, makadirio  ya  idadi  ya  watu  katika  Mkoa  wa Dar  es  Salaam kwa  mwaka  2016 yalikuwa ni  watu 5,465,420;  wanaume  2,661,979  na  wanawake 2,803,442.

Makadirio haya  yametokana  na  Sensa  ya  Watu  na  Makazi  ya Mwaka  2012  kwa  kutumia  mbinu  za kidemografia zinazohusisha mabadiliko katika viwango vya uzazi, vifo, uhamaji na uhamiaji katika ngazi ya taifa, mkoa na wilaya/halmashauri husika.

Mradi huo ulielezwa utazisaidia halmashauri tano za Ilala, Temeke, Kinondoni, Ubungo na Kigamboni ambazo zinaongezeko la watu na kukua kwa kasi.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk Grace Maghembe alisema Tanzania imejizatiti kufikia asilimia 40 katika uzazi wa mpango ifikapo mwaka 2020, hivyo uwapo wa mradi huo utasaidia kuongeza nguvu ya hatua iliyofikiwa sasa ya asilimia 32.

“Hatukatazi watu kuzaa, hapana. Uzazi wa mpango unamaanisha tuzae watoto tunaoweza kuwahudumia na mama apate muda wa kulea mtoto mmoja baada ya mwingine,” alisema.

Meya wa Jiji la Dar es Salaam,  Isaya Mwita alisema ni vizuri kila mtu kuwa na watoto wachache ili aweze kuwahudumia

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Janeth Mgamba alisema mradi huo   unalenga maeneo ya miji.

Post a Comment

أحدث أقدم