Askofu
wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amefutiwa kesi ya
kushindwa kutunza silaha baada ya upande wa mashitaka kushindwa
kuthibitisha mashtaka hayo, na kuamuru arudishiwe mkoba wenye silaha
yake.
Gwajima na wenzake watatu wamefutiwa mashtaka hayo mbele ya hakimu mbele ya Hakimu Mkazi Kisutu, Cyprian Mkehe.
Katika
kesi hiyo ambayo Gwajima alikuwa akisimamiwa na Wakili Peter Kibatala,
washtakiwa hao walikuwa wakidaiwa kuwa Machi 29, 2015 katika Hospitali
ya TMJ iliyopo Mikocheni A walikutwa wakimiliki Bastola aina ya Berretta
yenye namba ya siri CAT 5802 bila ya kuwa na kibali toka kwa mamlaka
inayohusika na silaha na milipuko.
Ilidaiwa
kuwa washtakiwa hao walifanya kosa hilo kinyume na kifungu cha 32 (1)
na cha 34 (1) (2) na(3) cha sheria ya Silaha na Milipuko sura ya 223
iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2010.
Pia,
walidaiwa kuwa siku ya tukio washtakiwa hao pia walikutwa wakimiliki
isivyo halali risasi tatu za bastola pamoja na risasi 17 za bunduki aina
ya Shotgun.
إرسال تعليق