Marekani imeilalamikia Korea Kaskazini,kwa kauli yake kuwa ina haki ya kuzitungua ndege za kivita za Marekani hata kama zipo nje ya anga la taifa hilo. Msemaji wa ikulu ya Marekani ya white house Sarah Huckabee Sanders, amewaambia waandishi wa habari kuwa kauli iliyotolewa na Waziri wa mambo ya kigeni wa Korea Kaskazini kwamba Marekani imetangaza vita,ni ya kipuuzi.
Kauli hiyo ya waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini ni kufuatia ujumbe wa Rais Trump kupitia ukurasa wake wa twitter,uliokuwa ukisema utawala wa Pyongyoung hauwezi kudumu kwa muda mrefu.
Akizungumza katika kituo cha mafunzo cha kimataifa mjini Washington,Waziri wa mambo ya nje wa Korea Kusini Kang Kyung-wha, amesema dunia inapaswa kupatiwa nafuu na maudhi ya Korea Kaskazini.
"Hakika, hii inaonyesha kuwa Korea kaskazini itaendeleza maudhi yake, na katika mazingira kama haya,sisi Korea Kusini na umoja wa mataifa tunapaswa kulishughulikia suala hili kwa umakini mkubwa,ili kutoendeleza hofu ya madhara ya kijeshi katika ukanda wetu.
Hatuwezi kuwa na vita nyingine katika ukanda wetu,hatuwezi kuwa na vita katika rasi ya Korea. Madhara yake hayawezi kuwa kwa bara la Asia tu,bali hata kwa kaskazini mashariki mwa Asia na jamii ya kimataifa kwa ujumla.Hatuwezi kuhatarisha usalama wa raia wetu,waliofanya kazi ya kujenga demokrasia kwa miongo saba sasa na ujenzi wa uchumi kutokana na vita vilivyowahi kutokea..")
Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Marekani Pentagon Kanal Robert Manning amesema iwapo Korea kaskazini haitaacha vitendo vyake vya kuudhi,watatoa idhini kwa Rais kuchukua hatua dhidi ya Korea Kaskazini. Naye Balozi China wa umoja wa mataifa Liu Jieyi amesema suala hili linaingia katika hatua ya hatari.
Korea Kakskazini mbali ya kuwekewa vikwazo,imeendelea na majaribio yake ya Nyuklia na makombora,kinyume na msimamo wa umoja wa mataifa
Post a Comment