Msuva asema ukweli alichoambiwa na Samatta kabla ya kupata timu nje

Winga wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayeichezea Difaa El Jadid ya Morocco Simon Msuva ndio aliyefunga magoli mawili ya Taifa dhidi ya Botswana katika mchezo wa kirafiki uliyopo katika kalenda ya FIFA.

Msuva ambaye ndio kwa mara ya kwanza anaichezea Taifa Stars baada ya kujiunga na club yake mpya ya Difaa El Jadid baada ya mchezo amekubali kuongea na waandishi wa habari na kueleza na kueleza kuwa Samatta alikuwa akimshauri na kumtia moyo.

“Namshukuru Mungu kwa hatua niliyopiga na nafurahi kurudi nyumbani kulitumikia Taifa langu kwa sababu nimetoka Tanzania na nimepata timu Morocco, kiukweli nje ni nje tukiangalia mfano Samatta ametoka wakati ambao kulikuwa hakuna mchezaji anacheza nje” - Msuva

“Samatta ametuonesha mfano flani sisi wachezaji wa nyumbani kwa upande wangu nimefurahi Samatta kuonesha njia wengine tunafuata na tumemfuata Samatta kwa wivu wa kimaendeleo, kwa nini yeye anafanya vizuri nje lakini wakati mwingine  Samatta huwa anatuambia kila mchezaji una uwezo” - Msuva

Post a Comment

Previous Post Next Post