Vyakula bora vinavyoondoa sura ya uzee


Maisha ya sasa hivi yamegubikwa na matumizi ya vipodozi vya kuzuia uzee hadi kufikia kiwango cha kuonekana kama ni chakula kuliko vitu vya urembo. Vipodozi hivyo huja kama creams, visafisha ngozi au serums.

Lakini ieleweke kuwa kutumia vipodozi vya kuondoa uzee juu ya ngozi hakuwezi kuwa mbadala wa chakula ambacho kinaboresha mwonekano na kutunza ngozi yako kuanzia ndani.

Chakula cha kuzuia kuzeeka haraka ndiyo kitu muhimu katika kuufanya mwili wako usizeeke haraka na katika kuulinda mwili wako kutokana na mionzi ya UV (ultra violet) ambayo ndio chanzo kikuu cha mistari na mikunyanzi juu ya ngozi yako. ungana nami leo kuona ni chakula gani kinasaidia kutunza mwonekano wako wa ujana. 

Chakula Chenye Vitamini C 
Utafiti uliofanywa kwenye kikundi cha wanawake wenye umri wa miaka zaidi ya 40 ulionyesha kwamba wanawake wanaotumia chakula chenye vitamini C zaidi walikuwa na mikunyanzi (wrinkles) kidogo zaidi na ngozi zao hazikuwa kavu ukilinganisha na wale ambao walitumia vitamini hiyo kidogo. Hii ni kwa sababu vitamini C ni antioxidant yenye nguvu inayozuia uharibifu wa seli na DNA za seli hivyo kulinda uzalishaji wa collagen ambayo ndiyo nguzo muhimu ya kulinda ngozi yako.

Unashauriwa basi upate angalau mg 75 za vitamini hii kwa siku. Kwa mfano unaweza kupata chungwa moja wakati wa kifungua kinywa na piliplili tano za njano ndani ya saladi kwenye mlo wako wa mchana. Chakula chenye vitamini C kwa wingi ni broccoli, strawberries, pilipili nyekundu, nyanya, tikitimaji, pomegranate n.k.

Chakula Chenye Protini
Tafiti zilionyesha kuwa wanawake waliotumia proteni zaidi walikuwa na wrinkles chache zaidi kwenye ngozi zao kuliko wale ambao walitumia proteni kidogo, hii kwa sababu proteni hutoa viungo muhimu katika ujenzi wa collagen.

Ili upate proteni unashauriwa kula nyama ya kuku isiyo na ngozi, sehemu nyeupe ya mayai na samaki. Unapochagua kula nyama ya ng’ombe au nguruwe, pendelea kutumia ile isiyo na mafuta sana. Matumizi ya soya yameonyesha kusaidia kuondoa ile mistari myembamba kweye macho.

Samaki Wenye Mafuta
Samaki wa baharini wenye mafuta wamebainika kuwa na kiwango kikubwa cha “omega-3 fatty acids”, kitu ambacho husaidia kuilinda ngozi yako kutokana na mionzi mibaya ya jua ambayo hudhoofisha collagen.

Nafaka Nzima
Utumiaji wa nafaka nzima badala ya wali mweupe, mikate inayotokana na ngano nyeupe na nafaka nyingine zilizokobolewa una faida nyingi. Moja ni kuzuia mwongezeko wa insulin katika mwili ambayo ina madhara ya kuharibu ngozi. Pia nafaka nzima ni chanzo cha madini ya selenium ambayo husaidia kuikinga ngozi yako kutokana na mionzi ya jua (UV rays).

Unashauriwa kutumia brown rice, shayiri na ngano nzima ili uweze kupata madini haya yatakayokusaidia kulinda ngozi yako.

Green Tea
Green tea ni kinywaji chenye antioxidants nyingi. Unywaji wa vikombe viwili au vitatu kwa siku wa chai hii utaifanya ngozi yako kuwa nyororo. Chai hii pia huzuia mikunyanzi isitokee kwenye ngozi yako.

Hatuwezi kuorodhesha chakula chote ambacho kinafaa katika kuzuia kuzeeka haraka katika ukurasa mmoja, hivyo makala yetu inatoa mwongozo tu wa namna ambavyo unaweza kupanga mlo wako. Usisite kutoa maoni yako kuhusu mada hii, tutafurahi mno kusikia kutoka kwako msomaji

Post a Comment

أحدث أقدم