Vituo vya afya bado kitendawili Karatu


Wananchi wa vijiji vinne vya kata ya Barayi wilayani Karatu mkoani Arusha wakiwemo wajawazito  wanalazimika kutembea umbali wa zaidi ya kilometa 100, kufuata huduma muhimu za Afya ikiwemo ya upasuaji  na wameiomba serikali kuwatatulia tatizo hilo wanalodai kuwa linahatarisha maisha yao

Wakizungumza na ITV iliyotembelea kata hiyo wananchi hao  wamesema licha ya kuwa na zahanati  inayotegemewa na watu zaidi ya Elfu ishirini (20'000) uwezo  wake  wa kutoa huduma ni mdogo  na wamekuwa wakipewa ahadi ya kujengewa Kituo cha Afya  ambayo bado haijatekelezwa.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Karatu, Waziri Morisi, amesema katika bajeti yao ya  2018/19   wameshatenga fedha zaidi ya Milioni mia moja kwa ajili ya  kujenga kituo cha Afya na ujenzi unatarajiwa  kuanza wakati wowote kuanzia  sasa.

Mwenyekiti wa  Halmashauri ya Karatu Bw. Jubilet Mnyenye amesema pamoja na mradi huo wa Afya pia wamepitisha  bajeti bilion  39.7 kwa ajili ya miradi ya maji, Elimu ,na miundombinu  ambayo ikikamilika itapunguza kero nyingi za wananchi hasa vijijini.

Post a Comment

Previous Post Next Post